Home Habari za michezo EHEE…MASTAA BONGO WAMVULIA KOFIA ‘BABU KAJU’…KAPOMBE KASHINDWA KUJIZUIA KAFUNGUKA HAYA…

EHEE…MASTAA BONGO WAMVULIA KOFIA ‘BABU KAJU’…KAPOMBE KASHINDWA KUJIZUIA KAFUNGUKA HAYA…

Ubora ulioonyeshwa na kiungo wa Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ katika mechi yao ya marudiano ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain, umewaibua mastaa mbalimbali wanaocheza Ligi Kuu Bara huku viungo wa Yanga wakimpigia saluti.

Sure Boy alianza kwenye mchezo huo na Yanga ilishinda bao 1-0 na kuonyesha uhai eneo la kiungo lililokuwa chini ya Khalid Aucho na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

“Tumepata matokeo mazuri na kutinga hatua ya makundi na mchezo unachezwa na wachezaji 11 uwanjani, lakini kulikuwa na kitu cha ziada kutoka kwa Sure Boy, alicheza mpira mzuri, aliiunganisha timu, nafurahia kucheza na kaka yangu, alikuwa bora sana kwenye mechi hiyo,” alisema Fei Toto.

Naye Aucho alisema; “Hongera kwake Sure Boy alikuwa na mchezo mzuri ukiachana na matokeo tuliyopata. Kwa upande wangu ndiye alikuwa mchezaji bora wa mchezo, palipokuwa panatakiwa kutoa pasi alitoa na sehemu ambayo hapakuhitaji uharaka alikaa na mpira na kuituliza timu, hiyo ndio sifa ya kiungo mzuri.”

Huku Yanick Bangala ambaye alicheza beki ya kati naye akisema; “Babu Kaju ni mchezaji mzuri na mkubwa, anajua kazi yake uwanjani, anastahili sifa anazopewa, alitusaidia kukaba na kutengeneza mashambulizi, nampongeza na kumtakia ubora huo uendelee kwenye mashindano ya ndani na kimataifa.”

Mbali na mastaa wenzake kutoka ndani ya Yanga hata wachezaji kutoka timu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu wametoa pongezi kwa staa huyo.

“Hongera sana kiungo na nahodha wangu wa mpira, ulikuwa bora sana na ulikuwa na mchezo mzuri hakika mmestahili ushindi mlioupata nakutakia maandalizi mema na kila lakhel kwenye michezo mingine ya kimataifa baada ya kutinga hatua ya makundi,” aliandika Price Dube mshambuliaji wa Azam FC.

“Fundi mwenye ufundi wake kafanya jambo eneo la kiungo ameupiga mwingi amewaficha wachezaji wa timu pinzani kwenye uwanja wao wa nyumbani amelifanya suala lililokuwa linachukuliwa kwa ugumu kuwa jepesi,” alisema Said Ntibazonkiza kiungo wa zamani wa Yanga ambaye sasa anakipiga Geita Gold.

Kiungo mkabaji wa Simba, Shomari Kapombe alimpongeza kiungo huyo ambaye ni mshikaji wake wa kitambo kwa kumwambia amefanya kile kilichokuwa kinatarajiwa na wanayanga.

SOMA NA HII  NABI AMCHOMOA MUKOKO SIMBA..NKANE ATISHIWA NA SIMU YANGA..SIMBA HII UNAPIGWA NYINGI...