Home Habari za michezo NABI BAADA YA KUSKIA SIMBA WAKO BENIN…KACHEEKAA KISHA AKASEMA HAYA…AOMBA DK 180...

NABI BAADA YA KUSKIA SIMBA WAKO BENIN…KACHEEKAA KISHA AKASEMA HAYA…AOMBA DK 180 TU…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ametenga mechi mbili za ligi ambazo ni sawa na dakika 180 kabla ya mchezo wao dhidi ya Simba kwa kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi kwa lengo la kupunguza presha katika mchezo huo utakaopigwa Aprili 30, mwaka huu.

Nabi ametenga dakika hizo katika mechi dhidi ya KMC ambayo itapigwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar kisha kucheza na Azam, Aprili 6, mwaka huu kabla ya kumalizana na Simba katika mchezo wa Aprili 30, mwaka huu.

Yanga kwa sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 45 baada mechi 17, ikifuatiwa na Simba wenye pointi 37 huku Azam wakiwa kwenye nafasi ya tatu na pointi 28.

Nabi alisema kuwa kama wanataka kupata matokeo makubwa katika mchezo dhidi ya Simba, wana kila sababu ya kuhakikisha wanashinda mechi zao mbili kabla ya mchezo huo.

β€œTuna mechi ngumu dhidi ya KMC ambao katika mzunguko wa kwanza tulifanikiwa kuwafunga lakini hatutegemei kuona mchezo kwamba utakuwa rahisi kwa kuwa sasa tunacheza kwenye mzunguko

ambao kila timu inapambana kwa kuhakikisha inapata matokeo makubwa ila malengo yetu yapo katika kushinda.

β€œNadhani kwa sasa ni muhimu kuangalia hizi mechi mbili tunapata ushindi halafu ndiyo tunaweza kuwa na mikakati ya kuwaangalia vizuri Simba, ingawa jambo ambalo tunaliangalia ni kuona tunashinda kwa kuanza na KMC kisha Azam kwa sababu tutakwenda kucheza bila presha dhidi ya Simba kwa kuangalia kupata ushindi pekee,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  CHAMA NA INONGA...WAINGIA KWENYE MTEGO WA RAJA CA