Home Habari za michezo ZA NDANIII KABISA…..HIZI HAPA SABABU ZA SIMBA KUWASIMAMISHA KIMYA KIMYA MASTAA WAKE...

ZA NDANIII KABISA…..HIZI HAPA SABABU ZA SIMBA KUWASIMAMISHA KIMYA KIMYA MASTAA WAKE WATATU..


Kocha wa Simba SC, Pablo Franco mjanja sana, kabla ya kuvaana na USGN ya Niger aliamua kuja na mkakati mzito kwa kuwachomoa nyota watatu wa kikosi hicho katika kambi ya timu hiyo, akiwamo nahodha John Bocco.

Mbali na Bocco wengine waliochomolewa kambini alikuwa beki Pascal Wawa na winga Jimmyson Mwanuke walioungana na Hassan Dilunga aliye majeruhi wa muda mrefu ambao ndio pekee waliokosekana kwenye kambi ya Simba iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa jumapili uliopigwa saa 4:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuibuka na ushindi wa 4-0 .

Tuanze na Bocco. Habari kutoka Simba zinasema kuwa nahodha huyo aliondolewa kambini kutokana na kupata majeraha, hivyo kocha akataka apate muda wa kutibiwa, wakati Wawa alizuiwa kwa kuchelewa kurudi kutoka kwao aliporuhusiwa.

Inaelezwa, Wawa aliomba ruksa kwenda Ivory Coast mara baada ya mechi ya Simba na ASEC Mimosas iliyopigwa Benin, lakini alichelewa kurudi na kuzuiwa kujiunga na kambi hiyo, kama ilivyokuwa kwa Mwanuke aliyeenda kwao kuweka sawa mambo ya kifamilia.

Winga huyo aliyesajiliwa msimu huu kutoka timu iliyoshuka daraja hadi Ligi ya Championship, Gwambina, mara baada ya kurudi alifanya mazoezi siku mbili ila timu ilipohamishwa kambi kutoka Mbweni kwenda Kisutu alienguliwa.

Kutokana na sababu hizo tofauti wachezaji hao kila mmoja alibaki nyumbani kwake baada ya benchi la ufundi kupendekeza wasiwepo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya USGN.

Mwanuke, alithibitisha hakuwepo kambini kutokana na kuomba ruhusa kwa ajili ya mambo ya kifamilia aliyokwenda kuyaweka sawa kabla ya kurejea kikosini katika majukumu yake ya kazi.

“Nilirudi kambini na nilifanya mazoezi siku mbili na wenzangu ila walikuwa tayari wamechanganya kwenye maandalizi kuna baadhi ya vitu nilikosa wakati ambao sikuwepo ndio maana niliondolewa,” alisema Mwanuke aliyecheza mechi ya duru la kwanza dhidi ya USGN kule Niger.

Kwa upande wa Dilunga aliye majeruhi, alisema anaendelea vizuri na jeraha lake la goti kwa matibabu anayopata na alisema alienda mazoezini kuwapa wachezaji wenzake hamasa kwa kuongea na kila mmoja aliyekuwepo.

SOMA NA HII  MAROUF TCHAKEI KUTUA SIMBA DIRISHA KUBWA...? UKWELI UNAOFAA KUJUA HUU HAPA...

“Nilivyokuwa awali baada ya kuumia na sasa ni tofauti kutokana na matibabu ninayopatiwa nikiwa chini ya uangalizi na gharama zote za Simba,” alisema Dilunga aliyejiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar. misimu mitatu iliyopita.