Home Habari za michezo KIUNGO MKATA UMEME WA SIMBA ATUA CHINA….DILI LAKE LIKO HIVI…

KIUNGO MKATA UMEME WA SIMBA ATUA CHINA….DILI LAKE LIKO HIVI…

Habari za Simba

Aliyekuwa Kiungo Wa Simba SC, Gerson Fraga Vieira raia wa Brazil amekamilisha usajili wake na kujiunga katika Klabu ya Tai Po ya nchini China.

Simba ilimsajili Fraga Juni 25, 2019 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea ATK ya Ligi Kuu India, akiwa miongoni wa Wabrazili waliosajiliwa msimu huo, akiwamo Tairone Santos na Wilker Henrique.

Brazili huyo aliachwa kwenye dirisha dogo la msimu uliopita baada ya kuwa majeruhi wa muda mrefu tangu alipoumia kwenye mechi kati ya timu yake na Biashara United iliyopigwa Septemba 20, mwaka jana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar na Simba kushinda mabao 4-0.

Jereha la goti lilimfanya mabosi wake kumtema na kumsajili Taddeo Lwanga kutoka Uganda ambaye naye kwa sasa ni majeruhi wa muda mrefu, huku ikielezwa kuwa huenda akatemwa jumla kwenye dirisha hili dogo la usajili na Mbrazili huyo kurejeshwa kikosini.

SOMA NA HII  BREAKING: CHAMA AMALIZA UTATA KUHUSU ISHU YAKE YA KURUDI TZ....AMTAJA SHOMARI KAPOMBE....