Home Uncategorized AMBULACE YAZUA KIZAAZAA LIGI KUU BARA

AMBULACE YAZUA KIZAAZAA LIGI KUU BARA


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Ruvu Shooting na Tanzania Prisons ambao ulipaswa uchezwe jana, Februari 11,2020 Uwanja wa Mabatini uliahirishwa na unasubiria maamuzi kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kujua kuwa kama utachezeka ama wageni watapewa pointi za mezani.

Sababu kubwa ya mchezo huo kushindwa kuchezwa ni kutokana na wenyeji Ruvu Shooting kushindwa kuwahisha gari ya kubebea wagonjwa, Ambulance ndani ya muda wa kuanza mpira.

Ambulance hiyo ilifika saa 10:34,waamuzi waliruhusu mchezo uanze lakini Tanzania Prosons waligoma kwa madai kuwa gari hiyo ilichelewa baada ya kuwasili nje ya dakika 30 kwa mujibu wa kanuni.

Mchezo huo jana uliahirishwa baada ya gari ya huduma ya kwanza (Ambulance) kuchelewa. Hivyo mchezo huo unasubiri maamuzi kutoka TFF kama utachezwa ama la.

SOMA NA HII  MBONA WATANYOOKA TU!! DE GEA WA YANGA KIMEELEWEKA CAF