Home Azam FC AZAM FC ITAWAFIKIA MASHABIKI WAO KIMATAIFA KWA MTIDO HUU

AZAM FC ITAWAFIKIA MASHABIKI WAO KIMATAIFA KWA MTIDO HUU


 LEO kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kitakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Horseed FC.

Ni mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na maelekezo kutoka Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) ikiwa ni kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Azam FC imeweka wazi kuwa mashabiki na wadau wa soka wataweza kuushuhudia moja kwa moja mchezo huo wa leo Jumamosi dhidi ya Horseed, kupitia Azam TV chaneli ya Azam Sports HD 1 kuanzia saa 1.00 usiku.

Pia Azam FC watatoa ripoti kwa kile ambacho kitajiri uwanjani, kupitia akaunti za mitandao yetu ya kijamii ya facebook (Azam Football Club) na Instagram (azamfcofficial), zote zikiwa na blue tick (verified).


Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria, amesema kuwa maandalizi ya mwisho yapo vizuri kwa kuwa kikosi kilishamaliza mazoezi na ni mchezo pekee unasubiriwa kwa sasa.

Pia kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 Azam FC iliweka kambi nchini Zambia na iliweza kucheza pia mechi za kirafiki.
Kipa wao namba moja Mathias Kigonya anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza leo.
SOMA NA HII  BAADA YA KUWATANDIKA BAKORA TZ PRISONS JANA....YANGA WAIFUATA NAMUNGO 'ASUBUHI ASUBUHI'...