Home news KARIA, SIMBA, WATANZANIA WAMLILIA HANS POPE

KARIA, SIMBA, WATANZANIA WAMLILIA HANS POPE

 


KUFUATIA taarifa za kutangulia mbele za haki kwa Zakaria Hans Pope aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugezi ndani ya Simba, wachezaji pamoja na vongozi mbalimbali wamekuwa wakimlilia kiongozi huyo.

Pia Pope enzi za uhai wake alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF).

Taarifa zake zimetangazwa usiku wa kuamkia leo na kwa wakati huu familia ya michezo pamoja na Tanzania kiujumla inazidi kumuombea kheri na kumuombea apumzike kwa amani.

Pia Rais wa TFF, Wallace Karia juu ya kutangulia mbele za haki kwa Zakaria Hans Pope aliyefariki katika Hospitali ya Aga Khan.

Mbali na Karia pia habari kutoka kambi ya Simba Arusha imeeleza kuwa wachezaji wote wamepatwa na mshutuko kutokana na taarifa hizo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameandika ujumbe huu:-“Leo moyo wangu ni mzito sana Mungu ailaze roho ya marehemu Zakaria Hans Poppe mahali pema peponi. May the Lord Almighty rest your beautiful soul in eternal peace ZHP. Mapenzi ya Mungu yatimizwe.” .

Pia Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema:”Ninamfahamu kwa miaka mingi akiwa ni Mwana Simba mahiri , mwenye msimamo na ukweli. Ni mtu aliependa umoja na kupata mafanikio kwa jumla. Siku zote alikubali kutumikia klabu kwa moyo wake wote , bila kujali muda wake, mali au hasaraā€¯.


SOMA NA HII  WAKIMBIA JOGGING WA TABATA WAFIKIWA NA MERIDIANBET....KAMA LINAKUHUSU...LINAWAHUSU...