Home Habari za michezo ALICHOSEMA MANARA BAADA YA KUPEWA KADI YA UANACHAMA WA YANGA…

ALICHOSEMA MANARA BAADA YA KUPEWA KADI YA UANACHAMA WA YANGA…


Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara amepatiwa rasmi kadi ya uanachama wa klabu hiyo.

Kadi hiyo iliyosajiliwa katika mfumo wa kielektroniki amekabidhiwa jana Aprili 28, 2022 na Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla.

“Hatimaye leo nimepata kadi yangu ya kwanza katika maisha yangu ya kuwa mwanachama kwenye klabu ya mpira nchini,” amesema Manara na kumshukuru Dk. Msolla na viongozi wengine, wadhamini na mashabiki.

Amesema yeye sasa ni mwanachama kamili wa Yanga, amepata amani ya moyo na jambo hilo limemuongezea nguvu kubwa katika kuitumikia klabu hiyo aliyojiunga nayo Agosti mwaka jana akitokea Simba ya Dar es Salaam.

SOMA NA HII  KWA HUYU KOCHA MTUNISIA ....SIMBA WASIPOBEBA UBINGWA WA AFRIKA...DUNIA ITAFIKA MWISHO...'MATIZI' YAKE SIO YA KITOTO..