Home Habari za michezo KWA HUYU KOCHA MTUNISIA ….SIMBA WASIPOBEBA UBINGWA WA AFRIKA…DUNIA ITAFIKA MWISHO…’MATIZI’ YAKE...

KWA HUYU KOCHA MTUNISIA ….SIMBA WASIPOBEBA UBINGWA WA AFRIKA…DUNIA ITAFIKA MWISHO…’MATIZI’ YAKE SIO YA KITOTO..


Kocha wa viungo Simba, Mtunisia Sbai Karim amesema wachezaji wa timu hiyo watakuwa wanaongezeka ubora, ufiti na utimamu wa miili kadri ambavyo mashindano yatazidi kuchanganya na hataki masihara.

Karim alisema mara ya kwanza alipokutana na wachezaji ilikuwa Misri wakati huo utimamu na ufiti wao haukuwa katika hali nzuri kama ilivyo baada ya kukaa nao katika kwa miezi miwili.

Alisema sio vyema kumuongelea kocha wa viungo aliyepita ila wachezaji kuishi katika timu bila ya kuwepo kocha wa viungo kuna mahala hali zao za utimamu wa miili hushuka siyo kama vile ambavyo wanatakiwa kuwa.

“Baada ya kufika niliwaeleza wachezaji nataka kuona kila mmoja anapokea yale mazoezi ambayo nampatia pamoja na kuyaheshimu kwa maana ya kuyatunza kwani ni jambo la msingi kwake na timu.”

“Niliwaeleza kuna vyakula wanatakiwa kula, zaidi wakiwa hapa kambini nawasimamia lakini hata katika maisha yao ya kawaida hawatakiwi kula vingi vile vyenye mafuta kwani ni rahisi kuongeza kilo.

“Baada ya maagizo hayo nilianza nao kwa mazoezi ya taratibu kulekule Misri na kambi ilivyomalizika nashukuru wengi walikuwa katika ufiti ambao nilihitaji kuona kutoka kwao.

 “Nikiwa nao hapa nchini naendelea kuwapatia ratiba mbalimbali za mazoezi yale ya uwanjani na gym ili kuhakikisha wanakuwa na ufiti zaidi na habari njema kwetu mwendelezo ni mzuri, ” alisema licha ya kwamba alikataa kuweka wazi mastaa ambao wako fiti zaidi kikosini.

Karim alisema ufiti wa wachezaji wa Simba uliopo wakati huu utaimarika zaidi katika siku za mbele kutokana na kile ambacho anawapatia wakiwa pamoja kambini na katika maisha ya kawaida.

“Utimamu wa miili kwa wachezaji wetu utasaidia mambo matatu – kutokuwa na majeraha ya mara kwa mara, wachezaji kupambana na kushindana katika nguvu zilezile dakika zote tisini pamoja na kocha kupata uwanja mpana wa kumtumia mchezaji yeyote anayemuhitaji kulingana na mahitaji ya mechi husika kwani wote watakuwa fiti,” alisema Karim.

“Tangu nimefika Simba nimekuwa nikifanya kazi vizuri na wachezaji pamoja na benchi la ufundi katika kutimiza majukumu yangu pamoja na usaidizi kwa kocha mkuu ili kuhakikisha kila mechi tunafanya vizuri.”

SOMA NA HII  VIDEO: REKODI ZA SIMBA KUELEKEA MCHEZO WAO WA LEO DHIDI YA KAIZER CHIEFS

Katika hatua nyingine kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi alisema anamfahamu vizuri Karim tangu wakiwa Tunisia ni miongoni mwa makocha wazuri wenye uelewa wa masuala ya mazoezi ya viungo.

“Karim ana uwezo katika kutimiza jukumu lake na anaweza kufanya kazi nzuri ya usaidizi kabla ya mechi, muda wa mechi yenyewe hata baada,” alisema Nabi.