Home Azam FC ZIKISALIA SIKU CHACHE KABLA KUKIPIGA NA YANGA…AZAM FC NA KOCHA WAO MSOMALI...

ZIKISALIA SIKU CHACHE KABLA KUKIPIGA NA YANGA…AZAM FC NA KOCHA WAO MSOMALI MAMBO BADO MAGUMU…


Ikiwa katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC, timu ya Azam FC jana imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Taifa Jang’ombe Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mmarekani mzaliwa wa Somalia, Abdihamid Moallin anayesaidiwa na jopo la Waspaniola itashuka tena dimbani keshokutwa Uwanja wa nyumbani wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam kumenyana na Arta Solar ya Djibouti kabla ya kuivaa Yanga wiki ijayo.

Azam ilipoteza michezo yake miwili ya Ligi msimu uliopita dhidi ya Yanga na kwa usajili waliofanya msimu huu wana kila dalili ya kutamba kuondoka na ushindi.

SOMA NA HII  WIKIENDI YA UTAJIRI INAANZA NA UTAJIRI KUPITIA MKEKA HUU WA KIBABE NA MERIDIANBET...