Home Burudani MANDONGA MTU KAZI AZIDI KUTEMBEZA VICHAPO…KAONEKA AAPA KUMUA AKICHEZA NAYE TENA ILI...

MANDONGA MTU KAZI AZIDI KUTEMBEZA VICHAPO…KAONEKA AAPA KUMUA AKICHEZA NAYE TENA ILI NAYEYE APATE UMAARUFU..


Usiku wa kuamkia leo August 28, Bondia Karim Mandonga ameibuka kidedea katika pambano la uzito wa kati kwa kumpiga Bondia, Sotii Mdudu kutoka Kigoma kwa Technical Knockout raundi ya 4 katika pambano la raundi 8.

Pambano hilo limechezwa katika ukumbi wa Kidyama Beach Resort Kigoma ikiwa ni takribani wiki moja tangu Mandonga atumie dakika 1 na sekunde 56 kumchakaza mpinzani wake Musa Omary usiku wa kuamkia Agosti 22, katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha Tamasha la kihistoria la Sensabika.

Kwa upande wake bondia aliyemchakaza Mandonga katika pambano la mwezi uliopita, Shabani Kaoneka ameendelea kuonyesha kuumizwa na mafanikio ya mpinzani wake;

“Mandonga akiomba pambano la marudiano namuua, kwa sababu kama nimempiga akawa tajiri kuliko mimi bora safari hii nimuue tu.” Shaban Kaoneka.

SOMA NA HII  LOMALISA ASHTUA YANGA...AFUNGUKA A-Z MPANGO WA SIRI WA YEYE KUTUA JANGWANI....