Home news DIRISHA DOGO..HII HAPA ORODHA YA MASTAA WA YANGA WATAKAOACHWA…

DIRISHA DOGO..HII HAPA ORODHA YA MASTAA WA YANGA WATAKAOACHWA…


KLABU ya Yanga itawaongezea mikataba mipya nyota wake zaidi ya watatu huku kocha Nasreddine Nabi akimuweka kiporo, Adeyum. Mbali na kuwaongezea mikataba mipya nyota hao akiwamo Zawadi Mauya, Kibwana Shomari, na Yassin Mustapha, timu hiyo itamtoa kwa mkopo Paul Godfrey ‘Boxer’.

“Boxer atakwenda aidha Mtibwa au Polisi Tanzania,” alisema kiongozi wa juu wa Yanga ambaye aliomba hifadhi ya jina. Alisema klabu hiyo ilipanga kuwaacha wachezaji wawili, Ditram Nchimbi na Adeyum Saleh wakati huu wa dirisha dogo.

“Kuhusu Adeyum, kocha alisema asiachwe kwanza ili amuangalie na atatoa uamuzi kama aondoke au abaki baada ya kurejea kutoka Rukwa,” alisema.

Alisema mara baada ya timu kuwasili Dar es Salaam, wachezaji ambao mikataba yao imekwisha na kocha amependekeza waongezewe mikataba mipya, watapewa dili jipya.

“Wapo wengi, wote tumefanya mazungumzo nao ambayo yamekamilika na mara watakaporejea Dar es Salaam watasaini mikataba mipya. Hivyo mpaka sasa mchezaji ambaye ameondoka ni Nchimbi, Adeyum alikuwa aondoke, lakini kocha ametaka kumuangalia zaidi,” alisema.

Kuhusu usajili mpya, alisema watakaoongezwa ni wachezaji wanne, akiwamo mmoja wa kigeni kutoka Ivory Coast ambaye atakuja kuwa mbadala wa Yacouba ambaye anauguza majeraha ya goti alilofanyiwa upasuaji. Yanga tayari imemalizana na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC na Dennis Nkane kutoka Biashara United.

“Kuna mchezaji mmoja mzawa ambaye bado mazungumzo yanaendelea, na Muivory Coast ambao mambo yameiva, lakini mchakato ukikamilika tutawaweka wazi na hao ndio watahitimisha usajili wa timu yetu wakati huu wa dirisha dogo,” alisema.

SOMA NA HII  KISA USAJILI WA CHICO....YANGA YA GSM YAVIMBA MBELE YA TP MAZEMBE YA KATUMBI...YAWEKA OFA NENE MEZANI...