Home news KISA USAJILI WA CHICO….YANGA YA GSM YAVIMBA MBELE YA TP MAZEMBE YA...

KISA USAJILI WA CHICO….YANGA YA GSM YAVIMBA MBELE YA TP MAZEMBE YA KATUMBI…YAWEKA OFA NENE MEZANI…


VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga wanapiga hesabu katika dirisha dogo la usajili lililofunguliwa jana, ili kuimarisha kikosi chao kwa bilionea wao, Ghalib Mohammed ‘GSM’ kuamua kumvimbia bilionea wa TP Mazembe, Moise Katumbi kwa kufika bei ya kung’oa winga matata anayeichezea timu yake.

Yanga imepanga kumchukua winga huyo wa kuiongeza chachu katika kikosi chao baada ya kuona eneo la winga ya kushoto ikikosa mtu sahihi hasa baada ya kuumia kwa Yacouba Songne, ikiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu wao, Nasreddine Nabi.

Inaelezwa kuwa, Ghalib alifanya kikao kizito na kocha wao Nabi katika hesabu za dirisha dogo na kocha ametaka kuletewa mtu wa maana atakayekuja kuziba nafasi ya Yacouba ambaye atamkosa kwa msimu mzima baada ya kuumia goti na kufanyiwa upasuaji nchini Tunisia.

Hesabu za Yanga kwa msimu huu ni kubeba ubingwa, hivyo pengo la Yacouba linaonekana kuisumbua akili ya Nabi na katika kuiboresha safu yake ya ushambuliaji ametaka mtu wa maana anayejua kutumia mguu wa kushoto.

Kwenye mafaili ya Nabi na GSM kuna jina la winga mwenye kasi na chenga Chico Ushindi, ambaye inaelezwa alipotajiwa Yanga tu, mwenyewe amekubali kila kitu kuja kuvaa jezi za njano na kijani, huku akitajwa kuwa ni winga teleza na mwenye akili nyingi katika kumiliki mpira na kufanya uamuzi sahihi kuliko Tuisila Kisinda na ndiye atakayekuwa pacha wa Jesus Moloko anayemiliki winga ya kulia kwa sasa.

Ushindi aliwahi kugomea kutua moja ya klabu kubwa hapa nchini, lakini uwepo wa mastaa wa Kikongomani ndani ya Yanga umemvutia na amewasilisha maombi ya kutaka kuondoka akitaka kuvunja mkataba.

Hata hivyo, maombi ya Yanga yamegomewa na Katumbi aliyewaambia anaweza kufikiria kumtoa kwa mkopo tu, ili aelekee Yanga lakini sio kumuuza na kinachomchanganya Ushindi ni fedha aliyowekewa mezani na GSM.

Ushindi hataki kuachia nafasi hiyo akidokezwa na baadhi ya mastaa wa Yanga kwamba akizembea kufosi usajili wake ili kuachana na Mazembe, basi nafasi hiyo itatua kwa staa mwingine Mkongomani ambaye pia Nabi ana jina lake.

SOMA NA HII  MMISRI KUAMUA MECHI YA HOROYA vs SIMBA...KWA KUTOA KADI TU ..HAJAMBO KWA KWELI...

Mmoja ya vigogo kutoka ndani ya Mazembe waliihakikisha Yanga kuwa Ushindi anataka kuja Yanga kurejesha nafasi yake ya kuitumikia timu ya Taifa ya DR Congo akijua kwamba akitua Jangwani atakuja kuwasha moto mkali utakaorejesha jina lake.

Ndani ya Yanga wanafikiria kukubaliana na hatua ya kumchukua kwa mkopo, huku wakipiga hesabu kuwa endapo watamchukua mpaka mwisho wa msimu itakuwa hatua nzuri huku wakifuatilia kupona kwa Yacouba ambaye ataanza mazoezi mwisho wa msimu.

“Kila kitu kipo sawa, GSM alitaka kumchukua jumla, lakini Moise amegomea akitaka amtoe aje kukipiga Yanga kwa mkopo kitu ambacho kimeafikiwa na vigogo wote, kwani hitaji la Yanga ni kuona ina mtu sahihi wa wingi ya kushoto,” kilisisitiza chanzo hicho kilichohifadhiwa jina.

Yanga ikimnasa Ushindi sio tu kwamba itakuwa imepata mtu bora wa kutokea kushoto ambapo pia winga huyo anajua kutokea kulia akiweza kutumia vyema miguu yote miwili.

Ushindi pia anajua kutengeneza krosi za kutosha sambamba na kufunga – ubora ambao utaiongezea nguvu Yanga inayopambana kurudisha heshima ya mataji msimu huu.