Home news KISA YANGA…SIMBA WAMFICHA CHAMA…UONGOZI WAFUNGUKA A-Z MCHAKATO ULIVYO…

KISA YANGA…SIMBA WAMFICHA CHAMA…UONGOZI WAFUNGUKA A-Z MCHAKATO ULIVYO…


UONGOZI wa Simba umetamba kuwa mipango yao ya usajili inakwenda vizuri katika dirisha dogo wakipanga kufanya kwa siri huku wakitamka kiungo wao wa zamani anayekipiga RS Berkane ya nchini Morocco, Clatous Chama huenda akawa mmoja wao.

Kauli hiyo wameitoa mara baada ya kuwepo tetesi za Yanga kuwepo katika mipango ya kuwania saini ya Chama katika usajili huo wa dirisha dogo ambalo limefunguliwa juzi.

Inaelezwa kuwa kiungo huyo ameomba mwenyewe mkataba wake kuvunjwa kutokana na kutokuwa na furaha na timu hiyo tangu amejiunga nayo katika msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ally Shatry alisema kuwa ngumu kwao kwa hivi sasa kuweka wazi usajili wao dirisha likiwa limefunguliwa juzi Alhamisi.

Shatry alisema kuwa, watatangaza na kuweka wazi mipango yao ya usajili mara baada ya kila kitu kukamilika kwa kila mchezaji aliyekuwepo katika mipango yao.

Aliongeza kuwa Simba ni timu kubwa, akijulikana mchezaji wanayemuhitaji ni lazima klabu nyingine zinahitaji saini yake, hivyo wataendelea na usajili wao kimyakimya.

“Niwaondoe hofu Wanasimba kuwa kila kitu kinachohusiana na usajili wetu kinakwenda vizuri kwa hivi sasa tunafanya siri.

“Kila kitu kitakapokamilika, basi tutaweka wazi katika usajili wetu wa dirisha dogo, lakini kwa hivi sasa uongozi unaendelea na mipango yake ya usajili kwa wachezaji wa ndani na nje ya nchi.

“Na kuhusiana na Chama huenda akawa ni kati ya wachezaji tutakaowasajili, lakini kikubwa tutafanya usajili wetu kutokana na mahitaji ya kocha wetu Pablo,” alisema Shatry.

SOMA NA HII  SIMBA KUIBUKIA CONGO LEO,WAWILI KUIKOSA AS VITA