Home Habari za michezo RAIS KENYATTA ATOA ZAWADI YA MILIONI MIANNE KWA ‘SIMBA NA YANGA’ ZA...

RAIS KENYATTA ATOA ZAWADI YA MILIONI MIANNE KWA ‘SIMBA NA YANGA’ ZA KENYA….


Mchezo wa watani wa jadi, Mashemeji Derby umemalizika kwa sare ya bao 1-1. Mchezo wa kibabe haswa wenye picha ya utani na ushindani wa kweli. Mchezo huo ulipigwa jana Jumapili dimba la Kasarani na kushuhudiwa na viongozi wakubwa wa serikali.

Mchezo huo huwa ulizikutanisha Gor Mahia na AFC Leopards. Ambapo kwa awamu hii wenyeji Gor Mahia wamevuna alama moja sawa na Leopards ingawa kwa Ingwe ni matokeo mabaya kwani sasa watalazimika kusubiri msimu mwingine kuja kuvunja historia ya kutoshinda dhidi ya Kā€™Ogalo kwa miaka sita iliyopita.

AFC Leopards walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Victor Omune kipindi cha kwanza lakini Gor Mahia wakasawazisha kupitia kwa Benson Omala.

Katika jambo la kipekee kwenye mechi hiyo, imehudhuriwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga, na Waziri wa Michezo Amina Mohamed.

Baada ya mchezo huo, Rais Kenyatta ametoa zawadi ya hela ya Kenya shilingi milioni 12 kwa kila mmoja (Mahia na Leopards) ambazo ni sawa na fedha ya kitanzania 240,676,253.

SOMA NA HII  MSIMU WA MWAKA KEESHO...TFF WAJA NA MASHINDANO MAPYA....TIMU SHIRIKI NI NNE TU....MZIGO WOTE HUU HAPA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here