Home Habari za michezo PAMOJA NA KUMFUNIKA MAYELE…GEORGE MPOLE AZIDI KUNG’ARA LIGI KUU…MINZIRO NAYE YUPO SANA…

PAMOJA NA KUMFUNIKA MAYELE…GEORGE MPOLE AZIDI KUNG’ARA LIGI KUU…MINZIRO NAYE YUPO SANA…


Mshambuliaji wa Geita Gold George Aman Mpole ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa mwezi April.

Mpole alifunga magoli mawili na kusaidia upatikanaji wa goli moja kwenye michezo mitatu iliyofanyika ndani ya mwezi huo

Wakati huo huo Kocha wa Geita Gold Fred Minziro ameshinda tuzo ya Kocha bora wa mwezi wa Ligi kuu ya Tanzania.

Minziro alipata Ushindi kwenye michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja ndani ya mwezi April, akiwashinda Mbwana Makata na Patrick Odhiambo alioingia nao fainali.

Modestus Mwaluka ameshinda tuzo ya meneja bora wa uwanja kwa mwezi April. Mwaluka ni meneja wa Uwanja wa Sokoine Mbeya.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MASHABIKI WA YANGA WAMEPOA KUELEKEA MECHI YA KESHO....NABI AIBUKA NA HILI KUHUSU AZIZ KI....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here