Home Habari za michezo KISA ‘CONNECTION’ ….MANARA AAMKA NA ‘SURE BOY’….AMWANDIKI UJUMBE HUU MZITO KWENYE INSTAGRAM…

KISA ‘CONNECTION’ ….MANARA AAMKA NA ‘SURE BOY’….AMWANDIKI UJUMBE HUU MZITO KWENYE INSTAGRAM…


Kutoka kwa Haji Manara; Alisoma Sekondari ya Ufundi Kaole kule Bagamoyo, kipindi hicho pia alikuwa akicheza Team moja maarufu miaka hyo ikijulikana kama African Winners huko huko katika Mji wa kihistoria zaid nchini.

Alikuwa fundi aliyetumika kama Midfielder namba nane, akiwa anasoma na Baba zangu wadogo na Shangazi zangu, na alikuwa akija kwetu kwa Bibi yangu kama rafiki wa Baba zangu Wadogo, maeneo ya Posta ya zamani Magofuni, Bwaga Moyo.

Ndipo nilipomfahamu Abubakar Salum, ambae Mwezi January 1986, Mtangazaji maarufu nchini miaka hyo Charles Hilary alipombatiza jina na kumwita Sure Boy.

Ilikuwa katika fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Ya kati, aliposawazisha Magoli mawili kwenye mechi baina ya Yanga na El-Merekh.

Ni kipindi hicho alipoanza kutumika kama Winga wa kulia kutoka eneo la kiungo, akiwapisha Nyota Wakubwa Mohamed Yahya Tostao, Dotto Lutta Mokili, na Muhidin Cheupe, waliotumika kama Viungo kwenye Tournament hyo, Tostao na Mokili waliletwa maalum Kwa ajili ya Michuano hyo,iliyokuwa maarufu miaka hiyo.

Huyo ni Baba Mzazi wa Salum Abubakar,mchezaji nnaemhusudu kupitiliza nchini, Rafiki yangu na Mdogo wangu pia ni Mtani wangu wa karibu Nadhani ushaelewa msomaji.connection yangu na hawa Sure Boy.

Hii hadithi sijawahi kumhadithia yoyote hata Sure wa sasa hajui Yes Sure Boy wa sasa ni zaidi ya Sure Boy wa zamani, alichozidiwa ni Speed na Target ya kufunga, akimzidi Dadie katika accuracy passes, juggling na skills.

Ninashukuru kuwa sehemu ya Watu niliowahi kuenjoy kuona kipaji cha Sure Boy, kwangu ni vile tu alichelewa kucheza Team kubwa na kuimbwa imbwa na Washabiki, lakini huyu ni Best Midfielder NambaNane kuwahi kutokea Tanzania, Kwa miaka kumi nyuma.

Kwa aliyepata kuniona mimi nikicheza Football hawezi kushangaa kwa nini nampenda Salum Abubakar.

Enjoy life Fundi wangu Sure Boy Junior, mimi nipo huku kitaa lakini nakushabikia mno. ???????????? @sure8boy

SOMA NA HII  USIMALIZE MWAKA KINYONGEE...KAMATA MCHONGO HUU WA UHAKIKA KUTOKA MERIDIANBET...