Home Uncategorized MTIBWA SUGAR YAELEZA KILICHOWAPONZA MBELE YA SIMBA

MTIBWA SUGAR YAELEZA KILICHOWAPONZA MBELE YA SIMBA


ZUBERI Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kilichoiponza timu yake kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Simba ni kushindwa kuwazuia wapinzani wake eneo la katikati ya uwanja.

Katwila alishuhudia mlinda mlango wake namba moja Shaaban Kado akiokota mipira nyavuni mara tatu kwa mabao ya John Bocco, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Hassan Dilunga.

“Tulikuwa bora na mipango yetu ilikuwa imara ila tulishindwa kuzuia eneo la katikati ya uwanja ambalo wapinzani wetu walitumia kutengeneza mipango yao,” .

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na ina pointi 23.

SOMA NA HII  M-Bet TANZANIA YATOA MAMILIONI KWA WATANZANIA WAWILI