Home Uncategorized DILUNGA AWAOMBA RADHI MABOSI WAKE WA ZAMANI MTIBWA BAADA YA KUWATUNGUA

DILUNGA AWAOMBA RADHI MABOSI WAKE WA ZAMANI MTIBWA BAADA YA KUWATUNGUA


HASSAN Dilunga, kiungo wa Simba ambaye alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar amesema kuwa anaomba radhi kwa mashabiki wake kwa kuwafunga moja bao kwenye ushindi wa mabao matatu.

Dilunga alifunga bao la tatu kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

“Nahitaji msamaha kwa mashabiki wangu wa Mtibwa na wachezaji wenzangu kwani nilikuwa nao zamani na bado naendelea kuwa nao kwenye maisha japokuwa kwa sasa nipo Simba na kazi yangu laimza niifanya kwa ukamilifu.

“Malengo yetu ni kuona mashabiki wa Simba wanafurahi huku tukiendelea kupambana kufikia malengo tuliyojiwekea,”. 

Simba imefunga jumla ya mabao 45 ambapo Dilunga amefunga jumla ya mabao sita.

SOMA NA HII  WALIOOA FC WACHEKELEA SAPOTI YA SALEH JEMBE