Home Uncategorized HIVI NDIVYO YANGA ILIPOKUBALI KULAZIMISHA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA MBEYA...

HIVI NDIVYO YANGA ILIPOKUBALI KULAZIMISHA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA MBEYA CITY


BERNARD Morrison, mshambuliaji wa Yanga, jana ameonyesha ushujaa wake mbele ya Mbeya City kwa kufunga bao kwenye sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.


Mbeya City walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 42 ambalo walilipata kupitia kwa beki wa Yanga, Lamine Moro ambaye alijifunga kwenye harakati za kuokoa mpira langoni mwao.

Kipindi cha pili Yanga waliongeza mashambulizi kupitia kwa Ditram Nchimbi aliyekuwa akitengeneza majalo mengi katikati Ila hayakuzaa matunda.

Dakika ya 78 Morrison aliweka mzani sawa kwa kichwa kikali akiwa kwenye msitu wa mabeki akimalizia pasi ya Juma Abdul.

Morrison anafunga bao lake la pili ndani ya ligi na kuwafanya Yanga wagawane pointi moja na Mbeya City iliyo chini ya Amri Said.

Kwenye mechi nyingine ya Ligi Kuu kati ya Ruvu Shooting na Tanzania Prison iliyotakiwa ichezwa Uwanja wa Mabatini iliahirishwa ikisubiri maamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na Ruvu Shooting kushindwa kuwahisha Ambulace ambayo ilichelewa kufika uwanjani.

Sare hiyo inaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 38 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
SOMA NA HII  KOCHA WA YANGA AZUIWA KURUDI TANZANIA NA MFALME WA UBELGIJI