Home Uncategorized KINACHOIBEBA AZAM FC HIKI HAPA NDANI YA LIGI KUU BARA

KINACHOIBEBA AZAM FC HIKI HAPA NDANI YA LIGI KUU BARA

IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kikubwa kinachowapa ushindi ni wachezaji kujituma ndani ya uwanja na ushirikiano wao.

Azam FC jana ilishinda mbele ya Polisi Tanzania bao 1-0 mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa wachezaji wanastahili pongezi na ana amini wataendelea kupambana kwenye mechi zao zote.

“Wachezaji wana juhudi uwanjani na wanastahili pongezi hicho ndicho ambacho kilicho nyuma ya ushindi wetu na mashabiki pia tunawaomba waendelee kutupa sapoti,” amesema.

Bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa na Mudhathir Yahaya dakika ya 49 kwa pasi ya Nicolas Wadada na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 44.

SOMA NA HII  MAJIMAJI HESABU ZAKE NI KUREJEA NDANI YA LIGI KUU BARA