Home news SIMBA YAONGEZA MZIGO WA JEZI MPYA SOKONI

SIMBA YAONGEZA MZIGO WA JEZI MPYA SOKONI


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kutokana na mahitaji makubwa ya jezi zao za msimu uliopita wa 2021/22, mzabuni na mbunifu wa jezi hizo kampuni ya Vunjabei wamelazimika kuongeza oda ya utengenezaji wa jezi hizo, ili kukidhi mahitaji wa mashabiki wa klabu hiyo kabla ya tamasha la Siku ya Simba ‘Simba Day’.

Simba inatarajia kufanya tamasha la siku ya Simba ‘Simba Day’ Septemba 19, mwaka huu ambapo pamoja na matukio mengine watatambulisha rasmi jezi hizo mpya watakazotumia kwa msimu ujao wa 201/22. 

Jezi za Simba zilianza rasmi kuuzwa Ijumaa ya wiki iliyopita na kuwa gumzo kubwa, ambapo kwa takwimu za Uongozi wa Simba ndani ya masaa nane ziliweka rekodi ya mauzo ya jezi kwa jezi 42,000 kuuzwa na kukadiriwa kuwa ziliingiza kiwango cha fedha kisichopungua Shilingi Bilioni 1.4.

Jezi hizo zinaendelea kuuzwa katika maduka ya Vunjabei pamoja na mawakala wake kote nchini ambapo jezi ya mtu mzima ni Shilingi 35,000 huku zile za watoto zikiwa zinapatikana kwa Shilingi 25,000.

Akizungumzia maendeleo ya mauzo ya Jezi hizo, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema: “Siwezi kuzungumza mengi kuhusiana na suala la mauzo ya jezi zetu mpya kwa sasa, kwa kuwa ni suala ambalo linashughulikiwa kwa kiasi kikubwa na mzabuni wetu kampuni ya Vunjabei.

“Lakini taarifa rasmi ambayo Uongozi umeipata kutoka kwa Vunjabei ni kwamba, mahitaji ya jezi yamekuwa makubwa hali ambayo imesababisha mzabuni kuongeza oda ya utengenezaji wa jezi hizo na kuzisafirisha, ili kufanikisha lengo na ahadi ya kila Mwanasimba kuvaa jezi mpya katika tamasha la siku ya Simba.”

SOMA NA HII  YACOUBA NDIO BASI TENA YANGA...KUUKOSA MSIMU MZIMA WA LIGI...SABABU HII HAPA...