Home news MTUNISIA MWINGINE ASHUSHWA YANGA KUMWAGA WINO

MTUNISIA MWINGINE ASHUSHWA YANGA KUMWAGA WINO


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi, 
ametoa mapendekezo kwa viongozi juu ya kuletwa kwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo ambaye ni raia wa Tunisia ambaye tayari wameshamalizana kila kitu na anatarajiwa kutua nchini wiki ijayo.

Yanga iliachana na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi ambao ni Kocha Msaidizi, Sghir Hammad mwenye uraia wa Tunisia, Kocha wa viungo Mmorocco, Jawab Sabri na Mchua misuli raia wa Afrika Kusini, Fareed Cassiem baada ya mikataba yao kumalizika.

Viongozi hao mara baada ya msimu uliopita kumalizika walienda mapumziko na baada ya hapo hawakujiunga na timu wakati ilipoenda nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya michuano mbalimbali kwa msimu ujao.

Kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Yanga walitambulisha wachezaji na benchi zima la Ufundi likiongozwa na Kocha Nabi huku mbadala wa Kocha wa viungo na mchua misuli wakionekana lakini kocha msaidizi akiwa bado hajapatikana.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa tayari kocha msaidizi ameshapatikana na atafika nchini hivi karibuni.

“Ni kweli kwa sasa timu haina kocha msaidizi lakini tumeshafanya mchakato na ameshapatikana, tunatarajia atakuja nchini kuanzia wiki ijayo kwa ajili ya kujiunga na timu.

“Ni raia wa Tunisia, tulimpata kutokana na mapendekezo ya kocha wetu mkuu, Nassredine Nabi na wanafahamiana vizuri hivyo tunatarajia mambo mazuri kutoka kwao,” alisema Mwakalebela.


SOMA NA HII  DAKTARI AANIKA KILA KITU KUHUSU AFYA YA KRAMO