Home Habari za michezo KOCHA MPYA YANGA KUTUA BONGO NA VYUMA VITATU VYA KAZI…MABOSI WAMPA ‘GO...

KOCHA MPYA YANGA KUTUA BONGO NA VYUMA VITATU VYA KAZI…MABOSI WAMPA ‘GO AHEAD’..

Kocha Mpya wa Yanga

KOCHA Mpya wa Yanga Miguel Gamondi anahesabu siku kabla ya kutua nchini kuanza kasi rasmi lakini mabosi wake wakamuachia nafasi tatu za kufanya maamuzi katika timu hiyo.

Mabosi wa Yanga wamemtega Gamondi wakimuachia nafasi ya kutafuta wasaidizi wake watatu katika benchi lake la ufundi wakiwemo kocha wa mazoezi ya viungo, kocha wa makipa na mtaalamu wa kuchambua mikanda ya wapinzani.

Nafasi hizo ziliachwa wazi kufautia kuondoka kwa Milton Nienov ambaye alikuwa kocha wa makipa, Helmy Gueldich aliyekuwa kocha wa mazoezi ya viungo na Khalil Ben Youssef aliyekuwa akifanya kazi ya kuchambua ubora wa timu pinzani kupitia mikanda ya video.

Yanga inataka kujiandaa na maisha mapya bila ya Khalil na Helmy ambaye alifanya kazi nzuri ya kuwapika wachezaji wa timu hiyo ingawa wenyewe bado hawajatoa jibu la moja kwa moja kwamba hawatarejea.

Inafahamika kuwa Gamondi endapo atawapata watu hao Yanga itafanya maamuzi ya haraka ya kuendelea na maisha bila ya makocha hao tayari kwa maandalizi ya mwanzo wa msimu mpya.

Gamondi anaweza kumkuta mwenyeji wake Cedric Kaze ambaye alikuwa msaidizi wa kocha aliyepita Nasreddine Nabi ambapo Mrundi huyo tayari ameshaonyesha hatua kubwa ya kukubali kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo.

“Kama ambavyo kocha aliyepita alikuja na watu wake na yeye (Gamondi) tumempa hiyo nafasi ashauri watu wa kuja nao tunachotaka awalete watu ambao watafanya kazi pamoja kwa ushirikiano siyo tumletee kisha baadaye wakaanza kupishana,” alisema mmoja wa mabosi wa Yanga aliyekuwa kwenye eneo zuri la maamuzi.

Tayari kocha huyo raia wa Argentina ameshawapa taarifa mabosi wa Yanga hana shida katika kuwapata wasaidizi wake hao ambapo wakati wowote atawajulisha juu ya majina aliyoyapata.

Siku chache zijazo kocha huyo raia wa Argentina anatarajiwa kutua hapa nchini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu ujao akiwa na hao wasaidizi wake.

Hivi karibuni kocha mzoefu kwenye soka la Afrika ambaye ameshatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu, Pitso Mosimane alisema ni vyema kwa klabu za Afrika kuajiri makocha wakuu na wasaidizi wao kwa kuwa ndiyo wanaweza kufanya kazi vizuri.

“Siyo jambo zuri kumuajiri kocha mkuu halafu akaja akawakuta wasaidizi, ukimpa kazi mwambie aje na wasaidizi wake, huyu anaweza kufanya kazi nzuri zaidi kwa kuwa wanajuana kwenye tamaduni zao,” alisema Pitso kocha wa zamani wa Al Ahly ya Misri.

SOMA NA HII  SENZO AFUNGA RASMI ISHU YA CHAMA NA YANGA...MUKOKO TONOMBE APELEKWA SIMBA SC...