Home Habari za michezo HUYU HAPA KIUNGO MMALI ALIYEMALIZANA NA SIMBA….MKATABA WAKE NI BALAA TUPU…

HUYU HAPA KIUNGO MMALI ALIYEMALIZANA NA SIMBA….MKATABA WAKE NI BALAA TUPU…

Habari za Simba leo

BAADA ya kumalizana na kiungo wao Jonas Mkude, uongozi wa Simba umeamua kuvunja benki na kumpa kiungo wao aliyekuwa amewagomea Sadio Kanoute mkataba wa miaka miwili.

Kanoute ambaye ameitumikia Simba kwa misimu miwili akitokea nchini kwao Mali amekubali kumwaga wino tena kwa miaka mingine miwili.

Chanzo cha taarifa hiyo kinasema awali Kanoute alitaka kuongezewa mshahara wake kutoka dola 8,000 sawa na shilingi milioni 19 hadi 10,000 sawa na shilingi milioni 23, jambo ambalo Simba waliona ni gumu, lakini wamejadili na kuamua kumpa mkataba.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa juzi walikubaliana na mchezaji huyo kuamua kusaini miaka miwili akiwa nchini kwao Mali.

“Kanoute alitaja pesa ambayo haikutarajiwa, sasa ilibidi apewe kazi Mels Daalder ambaye ni skauti mkuu ili azipitie kazi za mchezaji huyo kama atafaa kuisaidia klabu ndipo waanze kufanya makubaliano naye na naona kila kitu kimekwisha,” kilisema chanzo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia gazeti hili kuwa staa huyo tayari ameongeza makataba ataendelea kuitumikia timu hiyo hadi 2025.

Mbali na Sadio timu hiyo pia imemuongezea mkataba mshambuliaji wao Kibu Denis ambaye pia ataendelea kuwepo ndani ya timu hiyo kwa miaka miwili.

“Kibu na Kanoute wote wataendelea kuitumikia Simba kwa miaka miwili ilikuwa sio rahisi kuwaacha kutokana na kuwa miongoni mwa majina ya mapendekezo ya kocha;

“Bado zoezi la kuacha wachezaji na kuboresha timu linaendelea hii ni kutokana na kufuata ripoti ya kocha kuna baadhi ya wachezaji tunaendelea na mazungumzo nao kwa ajili ya kuvunja mikataba yao na wengine kuwabakiza hivyo muda wowote taarifa zitatoka.” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally alisema:

“Ripoti ya kocha imeonyesha wachezaji wanaowataka hivyo viongozi wanapambana na wachezaji ambao wanataka kubaki nao kwa ajili ya kupambania taji la ligi ambalo tumelikosa misimu miwili mfululizo.” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  SIMBA WALIAMSHA DUDE WATOA KAULI NZITO HUKO SUPER LEAGUE, SIO AL AHLY WA MAMELODI KAZI IPO HIVI