Home Habari za michezo DAKTARI AANIKA KILA KITU KUHUSU AFYA YA KRAMO

DAKTARI AANIKA KILA KITU KUHUSU AFYA YA KRAMO

Habari za Simba

Daktari wa Simba SC, Edwin Kagabo amesema nyota wa kikosi hicho, Aubin Kramo anaendelea vizuri na matibabu ya goti na kinachoendelea kwa sasa kwake ni taratibu mbalimbali ili kugundua ni lini atarejea uwanjani tena.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dk Kagabo amesema Kramo amesharudi baada ya kwenda, Ivory Coast kwa uchunguzi zaidi ila bado hajaruhusiwa kuanza mazoezi na wachezaji wenzake kikosini.

“Siwezi kuweka wazi ni lini atarudi kwa sababu kuna awamu ambazo sisi kama madaktari tumempa na tunaendelea kumfanyia uchunguzi hatua kwa hatua ingawa mashabiki wa simba watambue jeraha lake sio kubwa sana,” amesema na kuongeza madaktari wanaendelea kupamban ili kuhakikisha anarudi haraka iwezekanavyo kwani mashabiki wengi wa timu hiyo wanashauku kubwa ya kumuona akikitumikia kikosi hicho kutokana na ubora aliokuwa nao.

“Jeraha hilo la goti limekuwa likimsumbua mara kwa mara tangu ajiunge na timu, hivyo hivi sasa yupo katika hali nzuri baada ya kufanyiwa vipimo vya MRI na matumaini yetu atarudi mapema kuendelea na shughuli zake.”

Naye Daktari Shita Samwel akizungumzia jeraha la nyota huyo alisema; “Kuna aina tatu kwenye hizo nyuzi sasa unapoumia ukafanyiwa vipimo vya MRI ukagundulika zimekatika basi hiyo ina maana mchezaji anaweza akakaa nje kwa muda wa miezi sita hadi msimu mzima, lakini kama ni aina ya kwanza au ya pili kwenye hizo nyuzi kwa maana zimepishana kidogo tu na kusababisha huo utengano basi mchezaji atakaa nje kwa juma moja au mwezi mmoja.”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO