Home Habari za michezo SIMBA SASA KUPELEKA HASIRA ZAO ZOTE HAPA

SIMBA SASA KUPELEKA HASIRA ZAO ZOTE HAPA

Habari za Simba SC

Baada ya kupoteza kwenye mchezo wao uliopita wa ligi dhidi ya Simba hasira za Coastal Union zinahamia kwa Tabora United unaotarajiwa kuchezwa leo Septemba 29.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Coastal Union ilifungwa mabao 3-0 ikiwa ugenini dhidi ya mnyama Simba.

Mabao yote ya Simba yalifungwa na Jean Baleke ikiwa ni hat trick ya pili kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 ile ya kwanza ilifungwa na Feisal Salum.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mwinyi Zahera amesema kuwa kupoteza mchezo huo haikuwa mpango wao hivyo watafanyia kazi makosa yao mchezo ujao.

β€œKupoteza mchezo wetu dhidi ya Simba haina maana kwamba ulikuwa mpango wetu, sasa mipango ni kuelekea mchezo ujao ambapo tunahitaji ushindi na kupata pointi tatu.

β€œMakosa ilikuwa kipindi cha kwanza na tulizungumza na wachezaji kuongeza umakini kipindi cha pili ili kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa hilo liliwezekana,”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku na mchezo mwingine wa ligi unatarajiwa kuwa kati ya JKT Tanzania dhidi ya Kagera Sugar.

SOMA NA HII  PAMOJA NA RAHA ZOTE ZA MISRI...AKPAN AWA GUMZO KWA WAARABU...SHOW ZAKE ZA ZAGEUKA LULU...