Home Habari za michezo PAMOJA NA RAHA ZOTE ZA MISRI…AKPAN AWA GUMZO KWA WAARABU…SHOW ...

PAMOJA NA RAHA ZOTE ZA MISRI…AKPAN AWA GUMZO KWA WAARABU…SHOW ZAKE ZA ZAGEUKA LULU…

 


Wakati Simba ilipoanza kutangaza nyota wake wapya, mashabiki walipiga kelele, huku wengine wakiona kama walikuwa wakizungua kwani hawakuwa wakifanya mbwembwe kama timu nyingine, lakini mambo sasa ni tofauti kutokana na maandalizi yao huko Misri.

Kati ya wachezaji walionangwa usajili wao ni pamoja na Victor Akpan aliyetokea Coastal Union ya jijini Tanga, lakini moto aliouanzisha huko kambini Misri na namna alivyokiona kikosi cha Kocha Zoran Maki, kiungo huyo amewatumia salamu mashabiki akiwaambia; ‘Tulieni, utamu unakuja Msimbazi.”

Akpan alisema uwepo kwa majembe ya maana akiwamo Augustine Okrah na nyota wengine akiwamo yeye ni wazi Simba itafunika msimu ujao kuliko ilivyokuwa msimu uliopita.

“Hakuna kitu kizuri kama kutumia muda mwingi kujiandaa, halafu miguu yetu ndio iwe na kelele kubwa ikianza kufanya kazi ya kutimiza malengo ya klabu yetu,” alisema Akpan.

Alisema huko Misri kumenoga, kwa sababu wanajuana namna ya kucheza kitimu na kujiweka fiti, ili kuhakikisha wanaanza Ligi Kuu inayoanza Agosti 17 kwa kishindo.

Akpan alimwelezea Okrah kuwa ana uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira, ana kasi akiwa na mpira mguuni na ni mtu wa kujitenga sehemu ili kupewa mpira pamoja na jicho la kuona goli.

Akpan ameliambia Mwanaspoti kuwa amebahatika kucheza na Simba kabla ya kutua ndani ya timu hiyo anaona mabadiliko makubwa na yenye tija kwa ajili ya msimu mpya.

“Tupo kwenye maandalizi ya msimu mpya, wachezaji wengi ni wageni kutokana na kuingia dirisha hili la usajili kwa asilimia kubwa ni wachezaji wazuri kila mmoja anaonyesha uwezo wake, kocha atakuwa na wakati mgumu kupata kikosi cha kwanza,” alisema na kuongeza:

“Kwa mfano, wachezaji wa kigeni waliojiunga na timu hii wengi wao ni wazoefu kwenye mashindano ya kimataifa tuna deni kubwa kwa mashabiki na viongozi kuhakikisha tunaifikisha timu nusu fainali.”

Akpan alisema katika sajili zote zilizofanywa na timu hiyo amefurahia kucheza timu moja na Okrah ambaye anakiri ni mchezaji mzuri mwenye uchu wa mafanikio anamuona akifanya vitu vikubwa ndani ya timu hiyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA...'TRY AGAIN' ATOA AHADI YA KIBABE SIMBA..AFICHUA 'WALIVYOCHEZA KAMA PELE'..

“Okrah ametoka kwenye timu iliyokuwa inashiriki mashindano ya kimataifa alichokifanya kila mmoja anafahamu kwa upande wangu ni mchezaji mpambanaji na anajiamini,” alisema na kuongeza:

“Simba kwenye usajili wa Okrah wamelamba dume, atafanya mambo mengi makubwa kutokana na aina yake ya uchezaji, ni mchezaji ambaye hahofii mabeki anaingia ndani ya ‘box’ kwa kutumia nguvu na kasi.”

Wakati huo huo, Akpan alisema anaamini katika juhudi na kipaji alichonacho kuwa ana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

“Nimeamua kusajiliwa Simba sikuhofia kuwa kuna nani anacheza nafasi ninayocheza kwa sababu najiamini na naamini katika uwezo nilionao nisipocheza leo basi kesho nitacheza sijaja kukaa benchi,” alisema Akpan ambaye anacheza nafasi moja na wachezaji watatu aliowakuta kikosini kina Sadio Kanoute, Jonas Mkude pamoja na Taddeo Lwanga.