Home Uncategorized MEDDIE KAGERE AMTAJA ANAYEMUONGOZA KATIKA NJIA ZAKE

MEDDIE KAGERE AMTAJA ANAYEMUONGOZA KATIKA NJIA ZAKE

MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa kwenye kila jambo ambalo analifanya haachi kumuomba Mungu ili amuongoze kwani yeye ndiye kila kitu.

Kagere ni kinara wa kutupia mabao ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ametupia jumla ya mabao 13. Simba ikiwa imefunga mabao 47 yeye amehusika kwenye mabao 18, amefunga 13 na kutoa pasi tano za mabao.

Kagere amesema:”Katika kila jambo ambalo ninafanya siachi kumuomba Mungu kwanu yeye ndiye ambaye anatupa nguvu ya kufanya haya yote, ninawaomba mashabiki wanedelee kutupa sapoti,”.

Simba imecheza jumla ya mechi 23 msimu huu kwenye ligi imelazimisha sare mbili pekee mbele ya Tanzania Prisons bila kufungana na mbele ya Yanga kwa kufungana mabao 2-2.

SOMA NA HII  WACCHEZAJI WA TAIFA STARS WATAOKWEA PIPA KUELEKEA MISRI HAWA HAPA