Home Uncategorized SIMBA YATAJA SABABU YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

SIMBA YATAJA SABABU YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

HASSAN Dilunga, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa sababu kubwa itakayoipa Simba ubingwa ni jitihada za wachezaji kwenye mechi zao zote watakazocheza.

Dilunga amekuwa kwenye ubora wake chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck,amefunga mabao sita na kutoa pasi moja ya bao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Dilunga amesema wana kazi ngumu msimu huu ya kutwaa ubingwa jambo linalowafanya wachezaji kupambana uwanjani.
“Ushindani kwenye ligi ni mkubwa  na kila timu inapambana kufikia malengo, kitakachotupa ubingwa ni sisi wenyewe kupambana ndani ya uwanja na kupata matokeo mazuri hakuna kingine kinachohitajika.
“Mashabiki watupe sapoti kwani wao ni muhimu kwetu kufikia malengo ambayo tumejiwekea na kila kitu kinawezekana,” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 59 imecheza mechi 23 za ligi.
SOMA NA HII  NYONI: SIMBA ITAIFUNGA FC PLATINUM