Home Habari za michezo YANGA KUANZA KUTAMBULISHA VIFAA VIPYA LEO….MANARA AIBUKA NA STAILI YA SIMBA….MASTAA WAPYA...

YANGA KUANZA KUTAMBULISHA VIFAA VIPYA LEO….MANARA AIBUKA NA STAILI YA SIMBA….MASTAA WAPYA NI 5 TU…


Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema Yanga imesajili nyota watano wa kigeni ambao wataanza kuwatambulisha leo.

Akizungumza mara baada ya kuwasiri wakitokea Arusha walikocheza mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam na kutwaa taji kwa kumfunga Coastal Union kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-1 baada ya sare ya mabao 3-3.

Manara anasema wamesajili wachezaji watani tu wa kimataifa na wanaanza kumtambulisha mmoja lsaa 6 usiku.

“Ni wachezaji watano tu wa kigeni hatujasajili mchezaji yeyote mzawa na usiku wa kuamkia Jumatatu tuna mtangaza mmoja, kuamkia Jumanne, Jumatano mmoja hadi wanatimia watano,” anasema.

SOMA NA HII  PACOME, AZIZI KI, WAFANYA BALAA KUBWA YANGA