Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO…SIMBA NAO HAWAKO KINYONGEE AISEE…WAPANGA KUZIFUATA AL AHLY NA ZAMALEKI...

KUELEKEA MSIMU UJAO…SIMBA NAO HAWAKO KINYONGEE AISEE…WAPANGA KUZIFUATA AL AHLY NA ZAMALEKI MISRI…


MASTAA wa Simba wamepewa mapumziko ya siku 14, kabla ya kurejea tena kazini na fasta Julai 15 itakuwa ni safari ya kambini ambako ni Misri.

 Julai 15, kikosi cha Simba kitaondoka nchini kwenda Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi (Pre season) ya msimu ujao ambayo itakuwa si chini ya wiki mbili.

Awali uongozi wa Simba ulipanga kwenda kuweka kambi hiyo Afrika Kusini katika mji wa Johannesburg, ila imeshindikana kutokana na hali ya hewa ya huko kuwa ya baridi kali kipindi hiki, hivyo mabosi wakaamua iwe Arabuni, ila kwa kumpa kocha Zoran Maki achague nchini.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema wapo katika majadiliano, lakini timu yao msimu huu itakwenda kuweka kambi katika moja ya nchi za Afrika yenye asili ya kiarabu.

Try Again alisema watashauriana na Kocha Mkuu, Zoran Mako kuamua anataka kwenda wapi.

Alisema nchi moja wapo kati ya Morocco, Misri, Algeria na Tunisia wanaweza kwenda huko kutokana na vile ambavyo Zoran atakuwa anahitaji kwenye masuala yake ya kiufundi.

“Ukiachana na nchi hizo kuna moja ya Ulaya ambayo ni Uturuki kama ikitokea kuna changamoto au mabadiliko kwenye hizi za Afrika tunaweza kwenda huko kama ilivyokuwa misimu mitatu nyuma,” alisema Try Again na kuongeza;

“Timu itakuwa na mapumziko baada ya kujadiliana kuona mambo hayo ya kiufundi nchi gani yatapatikana kwa urahisi, upatikanaji wa vifaa, viwanja na vitu vingine vya msingi kama tiketi za ndege, usafiri na hoteli kwa pamoja tutakubaliana na kwenda huko.

“Wala hatuna hofu na usituone tupo kimya tunaendelea kwa mipango na mambo ya msingi kama yatakamilika kwa basi msimu ujao timu itafanya vizuri tofauti na msimu huu.”

Hata hivyo taarifa za ndani ya Simba zinasema kambi hiyo itakuwa Misri na hapo ndipo Zoran aliyechukua mikoba ya Pablo Franco atakapoliamsha dude kwa msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi hicho kilichopoteza mataji matatu.

SOMA NA HII  JINSI WAARABU WANAVYOLIHAMISHA SOKA KWAO....MESSI KAWACHOMOLEA NNJE MAPEMA TU..