Home Uncategorized MAJIMAJI HESABU ZAKE NI KUREJEA NDANI YA LIGI KUU BARA

MAJIMAJI HESABU ZAKE NI KUREJEA NDANI YA LIGI KUU BARA


 UONGOZI wa Klabu ya Majimaji umesema kuwa malengo yao makubwa kwa msimu huu wa 2020/21 ni kuweza kurejea ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.

Timu hiyo ilitolewa na Simba kwenye Kombe la Shirikisho kwa kufungwa mabao 5-0, Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Klabu ya Majimaji, Godfrey Mvula amesema kuwa wanatambua kwamba wamekosa Kombe la Shirikisho ambalo ilikuwa njia kwao kupeperusha bendera kimataifa watawekeza nguvu kwenye Ligi Daraja la Kwanza.

“Kwa sasa nguvu kubwa ipo kwenye Ligi Daraja la Kwanza ambapo tunahitaji kufanya vizuri ili kurudi kwenye ushindani kama livyokuwa zamani.

“Jukumu letu viongozi ni kusimamia mambo yaliyopo yaweze kwenda sawa huku tukiomba sapoti ya mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kila saa kila wakati,” amesema.

Ndani ya Ligi Kuu Bara kilishuka msimu wa 2017/18 na kwa sasa kinapambana ndani ya Ligi Daraja la Kwanza.

SOMA NA HII  VIDEO: BONDIA MBONGO ALIYEPIGWA TKO AUSTRALIA AFUNGUKA A-Z