Home Habari za michezo FT: SIMBA 2-0 ST GEORGE….KIBU NA OKWA WAFUNGA STAILI MOJA….CHAMA AMERUDIII..HUYO MZUNGU...

FT: SIMBA 2-0 ST GEORGE….KIBU NA OKWA WAFUNGA STAILI MOJA….CHAMA AMERUDIII..HUYO MZUNGU LABDA ‘WAMLOGE’…


SIMBA imeshinda mabao 2-0 dhidi ya St George kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni mchezo maalumu kwenye kilele cha Wiki ya Simba ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Zoran Maki ambaye ni raia wa Serbia.

Mabao ya Simba yamefungwa na mzawa Kibu Dennis na Nelson Okwa ambaye aliingia kipindi cha pili akitokea benchi.

Maki amesema kuwa wamefurahi kupata ushindi kwenye mchezo wa kirafiki na wanakwenda kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa,Agosti 13.

“Tunajua kwamba mchezo ulikuwa mzuri na wachezaji wameweza kufanya kikubwa bado kuna kazi ya kuweza kufanya ili kuweza kuongeza kitu kwenye kikosi chetu,”.

SOMA NA HII  BILA KUPEPESA MACHO...MECKY MEXIME AMPA TUZO YA MCHEZAJI BORA BANGALA...SABABU YAKE NI HII TU...