Home Habari za michezo #SIMBADAY: SIMBA WALIVYOIGARAGAZA YANGA KWA MKAPA LEO….MBABE WA MANDONGA AIBUA SHANGWE UWANJA...

#SIMBADAY: SIMBA WALIVYOIGARAGAZA YANGA KWA MKAPA LEO….MBABE WA MANDONGA AIBUA SHANGWE UWANJA MZIMA…


Tumeujaza! ndivyo wanavyosema mashabiki wa Simba baada ya kufanya kufuru kwenye tamasha lao la Simba Day ambalo kilele chake ni leo Agosti 8, 2022.

Licha ya idadi ya mashabiki wa Simba kuwa kubwa nje tayari uwanja umejazwa huku vaibu la tamasha likiendelea kupamba moto kutokana na burudani zinazoendelea.

Ni wazi mashabiki wa Simba wameipiga bao Yanga ambao licha ya kuwa wengi walishindwa kuujaza uwanja.

Ngoma kali na ustadi wa Dj Joozey vilionekana kuwakosha mashabiki wa Simba waliopo kwa Mkapa. 

KAONEKA ATEKA ‘SHOW’


Bondia mbabe wa Karim Mandonga, Shaban Kaoneka ametambulishwa katika kilele cha Tamasha la “Simba Day” linalofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kaoneka alimtandika bondia maarufu kwa sasa Karima Mandonga kwa TKO ya raundi ya nne Julai 30 katika Uwanja wa Maji Maji Songea.

Kwa maana hiyo Shaban Kaoneka nae mnyama.

SOMA NA HII  UZI MPYA WA SIMBA 2021/22 HUU HAPA