Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAINGIA SOKONI KUSAKA MAJEMBE YA KAZI

RUVU SHOOTING YAINGIA SOKONI KUSAKA MAJEMBE YA KAZI


 UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kwamba wakati huu wa dirisha dogo la usajili itaongeza majembe ya kazi mawili kwenye safu ya ushambuliaji ili kuongeza kasi ya kikosi hicho.


Chini ya Kocha Mkuu, Charles Mkwasa ambaye ana tuzo ya mwezi Novemba akiwa ni kocha bora kilipindua meza kibabe mbele ya Azam FC na kufanya matokeo kukamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.


Kwenye mchezo huo Ruvu Shooting ikiwa ugenini, Uwanja wa Azam Complex ilipata nafasi nyingi ambazo ilishindwa kuzitumia jambo ambalo limemfanya Mkwasa kufikiria kuongeza majembe ya kazi.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa lazima wafanye usajili ili kuongeza makali ya kikosi hicho.


“Kikosi kinacheza mpirampira wenyewe ule kama wa Barcelona hiyo ipo wazi, sasa kwa wakati huu nasi ni lazima tufanye usajili wa maana.


“Tayari ripoti inaonyesha kwamba tunahitaji kuongeza mshambuliaji na kuna sehemu nyingine za kuboresha kwenye ulinzi na kila kitu sisi tunajambo letu na hatushindwi.


“Ukitaka kuwajua ni wachezaji wapi wanasajiliwa subiri kwanza kila kitu kitakuwa sawa. Mashabiki waendelee kutupa sapoti,” .


Ruvu Shooting ipo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza michezo 16. Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 15 na ile ya ulinzi imeruhusu mabao 10.

SOMA NA HII  NYOTA WA SIMBA, BERNARD MORRISON NJE YA UWANJA MIEZI SITA