Home Uncategorized AZAM YAMFUATA MRITHI HUYU WA DAVID KISSU

AZAM YAMFUATA MRITHI HUYU WA DAVID KISSU


 KIPA namba moja wa Klabu ya Biashara United, Daniel Mgore amesema kuwa amefuatwa na mabosi wa Azam FC wakimuuliza kuhusu mkataba wake.


Nyota huyo ambaye ni chaguo namba moja kwa Kocha Mkuu Francis Baraza amekuwa akitajwa kuingia kwenye rada za Azam FC kwa muda mrefu ili akaongeze ujuzi kwenye chuo cha kukuzia vipaji kwenye ardhi ya Bongo.

Mgore anatajwa kuingia kwenye rada za Azam FC ili akarithi mikoba ya kipa namba moja David Kissu ambaye amekuwa akifanya makosa yanayolingana na ya kipa namba mbili Benedict Haule. 

Azam FC imeweza kutengeneza wachezaji wengi wazuri na imekuwa na makipa makini wanaofanya vizuri wakitoka hapo ikiwa ni pamoja na kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula.


Pia Metacha Mnata kipa namba moja wa Yanga naye pia amepita pale kwenye viunga vya Azam Complex kisha akaibukia Mbao FC ambapo alipata tuzo ya kipa bora kwenye mashindano ya Sport Pesa Cup.


Mgore amesema:”Kuna watu kutoka Azam FC ambao waliwahi kunifuata na kuuliza kuhusu mkataba wangu, hivyo niliwaambia kwamba wanapaswa wazungumze na uongozi wangu mimi sina tatizo na kipaji changu.


“Imani yangu ni kwamba nikipata changamoto mpya nitaimarika zaidi ya hapa. Ni jambo la kusubiri na kuona itakuaje,” .


Kuhusu ishu hiyo ya mgore kuibukia Azam FC, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit hivi karibuni aliweka wazi kwamba hakuna mpango wa kuipata saini yake.

SOMA NA HII  ISHU YA NYOTA WA YANGA KUIBUKIA IHEFU YABUMA