Home Uncategorized JUHUDI YA WACHEZAJI YANGA YAMKOSHA KAZE

JUHUDI YA WACHEZAJI YANGA YAMKOSHA KAZE


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa vijana wake wamekuwa na juhudi isiyo ya kawaida ndani ya uwanja jambo ambalo linawapa urahisi kupata matokeo ambayo wanahitaji ndani ya Ligi Kuu Bara.

 Vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 43 wamekamilisha mzunguko wa kwanza kwa kucheza mechi 17 bila kupoteza mchezo zaidi ya kuambulia sare.


Imeshinda jumla ya mechi 13 na kupata sare nne ndani ya mzunguko wa kwanza huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 28.


Ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine ulihitimisha mzunguko wa kwanza kwa timu hiyo kukamilisha jambo lao la kucheza mechi zote za mzunguko wa kwanza na historia ya bila kupoteza.


Kaze amesema:”Ni jambo zuri kuona kila mchezo unakuwa na utofauti, ujue hawa wachezaji wanajua wanahitaji nini na ndio maana wakiwa ndani ya uwanja wanapambana.


“Ninapenda juhudi yao haina ukawaida kila wakati kila saa wanahitaji pongezi katika hilo ila kazi bado ipo,” .

Ihefu kipigo hicho kinaifanya iwe nafasi ya 17 na pointi zake ni 13 nayo pia imemaliza mzunguko ikiwa kwenye nafasi ya hatari ya kushuka daraja ikiwa haitabadili gia mzunguko wa pili.


Mikono ya kipa namba moja wa Ihefu, Deogratius Munish,’Dida’ ambaye ni ingizo jipya akiwa ni mchezaji huru ilikutana na balaa la Deus Kaseke, Yacouba Songne na Feisal Salum ambao walimtungua akiwa langoni.

SOMA NA HII  LEO SAMATTA KUKIWASHA TENA, USO KWA USO NA MSHIKAJI WAKE GUARDIOLA