Home Uncategorized YANGA WAPATA MTEREMKO KOMBE LA SHIRIKISHO, SINGIDA UNITED MAJANGA

YANGA WAPATA MTEREMKO KOMBE LA SHIRIKISHO, SINGIDA UNITED MAJANGA


SASA ni rasmi kuwa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze imetinga hatua ya nne bila kuingia ndani ya uwanja kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Yanga ilipaswa kuchezwa na Klabu ya Singida United ambayo ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza, Desemba 26 kutokana na timu hiyo kushushwa madaraja mawili sambamba na matokeo yake kufutwa mchezo huo hautachezwa.


Adhabu hiyo kwa Singida United imetokana na timu hiyo kushindwa kutokea uwanjani kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Alliance FC.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) leo Desemba 24 imesema:”Kufuatia Klabu ya Singida United kushushwa madaraja mawili, mchezo wa Azam Sports Federation (ASFC) namba 65 kati ya Young Africans v Singida United uliokua uchezwe Jumamosi Desemba 26, 2020 hautakuwepo,.


“Hivyo Young Africans sasa wanasubiri kucheza raundi ya nne 2021,” .

SOMA NA HII  DABO AKAZA NA AZAM AFUNGUKA HAYA KUHUSU MECHI DHIDI YA YANGA