Home Azam FC DABO AKAZA NA AZAM AFUNGUKA HAYA KUHUSU MECHI DHIDI YA YANGA

DABO AKAZA NA AZAM AFUNGUKA HAYA KUHUSU MECHI DHIDI YA YANGA

Kocha Mpya Azam FC

WAKATI Azam ikiwa mgeni wa Yanga kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kocha wa kikosi hicho, Youssouph Dabo amesema licha ya ugumu uliopo ila sababu itakayowapa ushindi ni nidhamu kwa wachezaji kuanzia kujilinda hadi ushambuliaji.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam, Dabo alisema Yanga ni timu bora ambayo wanaiheshimu kwa kiasi kikubwa, lakini wamejipanga kuhakikisha wanaendeleza rekodi nzuri ya kutopoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara katika msimu huu.

β€œSio rahisi unapocheza na timu kama Yanga kwa sababu ina wachezaji wazuri ambao tayari wameonyesha ubora mkubwa msimu huu, hivyo kwetu ni kipimo sahihi cha kuonyesha ni kwa jinsi gani tunahitaji kufikia malengo tuliyojiwekea,” alisema.

Dabo alisema kitendo cha mchezo huo kuondolewa katika Uwanja wa Azam Complex na kuhamishiwa Benjamin Mkapa hakitawaathiri wachezaji wa timu hiyo licha ya kuzoea mazingira ya nyumbani ambako ndiko wamekuwa na matokeo mazuri kwa asilimia 100.

β€œKama nilivyosema mwanzoni huu mchezo haujalishi unachezea wapi kwa sababu tunakutana na timu bora. Jambo la msingi na la muhimu ni maandalizi mazuri ya kiuchezaji kwa maana ya kucheza kwa tahadhari ya kujilinda na kutumia vizuri nafasi.”

Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa Agosti 9, mwaka huu katika Ngao la Jamii ambapo Azam ilipoteza mabao 2-0 huku kwenye Ligi Kuu Bara ikifungwa 3-2, Desemba 25 mwaka jana, mechi iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  MIEZI KADHAA BAADA YA KUACHANA NA YANGA...NTIBAZONKIZA AVUNJA UKIMYA...AIBUKA NA HAYA MAPYA...