Home Habari za michezo ALIYEKUWA KOCHA WA YANGA, NABI ATUA FAR RABAT YA MOROCCO

ALIYEKUWA KOCHA WA YANGA, NABI ATUA FAR RABAT YA MOROCCO

Aliyekuwa kocha wa Yanga Nasreddine Nabi amesaini mkataba wa miaka miwili kuwafundisha Mabingwa wa Ligi Kuu ya Morocco FAR Rabat.

Nabi amesaini mkataba huo jana kuwafundisha Mabingwa hao wa msimu huu nchini humo ikiwa ni miezi michache tangu aachane na Yanga.

Nabi amesema ni heshima kwake kupata nafasi ya kuifundisha klabu hiyo kubwa Afrika ambapo anataka kuhakikisha anatumia taaluma yake kuipa mafanikio zaidi.

“Ni changamoto mpya kwangu, FAR Rabat ni klabu kubwa Afrika kunipa nafasi ya kufanya kazi hapa ni heshima kubwa kwangu,naamini ni wakati mzuri kwetu kushirikiana kuipa mafanikio zaidi klabu hii,”amesema Nabi.

Akiwa Yanga Nabi ameiacha timu hiyo ikiwa na heshima kubwa akiwapa mataji yote ya ndani kwa misimu miwili mfululizo lakini pia msimu uliopita akiifikisha kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  MAXI NZEGELI KWA YANGA SASA HIVI NI ZAIDI YA SHUJAA