Home Habari za michezo KWA MUJIBU WA KANUNI SASA MAMLAKA ZITANGAZE RASMI YANGA IMESHUKA DARAJA…

KWA MUJIBU WA KANUNI SASA MAMLAKA ZITANGAZE RASMI YANGA IMESHUKA DARAJA…

Habari za Yanga

Kanuni za ligi kuu zinatamka wazi kwamba timu ikishindwa kusajili timu ya chini ya umri wa miaka 20 basi timu hiyo itaondolewa ligi kuu na kushushwa daraja.

Yanga haikusajili timu ya chini ya umri wa miaka 20 mpaka dirisha linafungwa.

Baada ya kugundua wamefanya kosa na adhabu yake ni kushushwa daraja Kwa kushirikiana na afsa mmoja wa Tff ambaye ni mwanachama wao wakafoji Kwa kutafuta baadhi ya wachezaji wa Moro Kids na kwingineko wakawapa leseni nje ya muda.

Hili lilithibitika wakati wa kikao Cha pree metch meating Cha mechi kati ya Simba under 20 na Yanga under 20. Simba waligomea kucheza hiyo mechi Kwa kuwa mpaka muda wa usajili unamalizika Yanga haikuwa imesajili Mchezaji hata mmoja wa under 20. Ili kufunika kombe mwanaharamu apite wenye mamlaka badala ya kuzifanyia kazi hoja za Simba kugomea mchezo wakaja na tamko la kuahirisha mechi. Ukweli ni kwamba mechi haikuahirishwa bali Simba waligomea mchezo.

Jambo zuri ni kwamba sistim ya usajili ipo wazi.
Tarehe na muda ulipofanyika usajili wa kugushi na magumashi vinaonekana. Kwa nini tunataka kupindisha kanuni?

Yanga ni waumini wazuri sana wa kanuni. Na wamejitanabaisha hivyo. Waliwahi kugomea muda wa mechi Kwa kutaka kanuni ziheshimiwe. Kwa sababu hizo hizo na hili wanapaswa kuziheshimu kanuni.

Kanuni ipo wazi kabisa kwamba muda wa usajili ukimalizika na iwapo timu haikusajili kinachofuata ni kushushwa daraja. Kama kweli tunaupenda na kuuheshimu mpira bila kujali ukubwa wa timu ni lazima kanuni zichukue mkondo wake.

Na afisa wa Tff aliyeshiriki hii dhambi anajulikana. Ni lazima na Yeye awajibishwe Kwa kufoji. Kwa nini alipitisha usajili nje ya muda? Kwa nini aliamua kufanya dhambi kuinusuru timu yake aipendayo?

Hapa huyu afsa ameudhalilisha mpira.
Ameidhalilisha Tff na anastahili adhabu. Kama tunataka kuulinda mpira na kuheshimu taratibu zake basi ni muhimu kwenye hili kanuni, sheria na taratibu zikaheshimiwa.

(Haya ni maoni na mtazamo wa Ndg. Jicho la tatu la Mgalilaya).

SOMA NA HII  YANGA MAMBO YAZIDI KUWA 'BAMBAM'...KUANZIA MWAKANI KUANZA KUVUNA MABILIONI YA UWEKEZAJI....