Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO Vs NAMUNGO YA MGUNDA….’NONDO’ KALI ZA SIMBA HIZI...

KUELEKEA MECHI YA KESHO Vs NAMUNGO YA MGUNDA….’NONDO’ KALI ZA SIMBA HIZI HAPA…

HABARI ZA SIMBA LEO

KOCHA Msaidizi wa Simba, Darian Wilken amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Namungo utakuwa mgumu lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi kwenye uwanja wa nyumbani.

Kocha Wilken amesema Namungo ni timu nzuri hasa ikichangiwa na kuwa na kocha mpya, (Juma Mgunda) ambaye amewaongezea moral wachezaji wake lakini itakutana na wapinzani bora zaidi yao.

“Utakuwa mchezo mgumu, Namungo ni imara yenye wachezaji wazoefu na tayari imepata kocha mpya, lakini Simba ni kubwa zaidi na ipo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajiili ya kupata pointi tatu,” amesema Kocha Wilken.

Amesema ratiba ni changamoto wanalazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji. Timu kubwa inajianda kupitia nyakati ngumu ili kuonyesha ukubwa wao.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kipa wa Simba, Ally Salim amesema kwa upande wao wapo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajili ya kupata pointi tatu.

Amesema Namungo ina wachezaji wazoefu ambao wengi walikuwa nao lakini Simba ni kubwa na pamoja na changamoto zote wapo tayari kwa ajili ya pointi tatu muhimu nyumbani.

“Tupo tayari kwa mchezo , Namungo tuna waheshimu ni timu bora lakini Simba ni bora zaidi na tupo kwa ajili ya kupigania alama tatu,” amesema Ally Salim.

SOMA NA HII  NYOTA HAWA WATATU WA SIMBA KUIKOSA YANGA KIGOMA