Home Simba SC NYOTA HAWA WATATU WA SIMBA KUIKOSA YANGA KIGOMA

NYOTA HAWA WATATU WA SIMBA KUIKOSA YANGA KIGOMA


WAKATI kesho kikosi cha Simba kikitarajiwa kumenyana na watani zao wa jadi, Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, kitawakosa nyota wake watatu.

Mchezo wa kesho, Julai 25 Uwanja wa Lake Tanganyika ni wa fainali na mshindi atasepa na taji hilo ambalo bingwa mtetezi ni Simba.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Ddier Gomes ilitwaa taji hilo msimu uliopita kwa ushindi kwenye fainali dhidi ya Namungo iliyokuwa inanolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery.

Kwa mujibu wa meneja wa Simba, Patrcik Rweyemamu ni nyota watatu ambao hawapo kwenye msafara wa kikosi ambacho kipo Kigoma.

Nyota hao ni Jonas Mkude ambaye ni kiungo mkabaji, Perfect Chikwende huyu ni kiungo mshambuliaji sawa na Ibrahim Ajibu.

Kuhusu maandalizi, Rweyemamu amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanahitaji ushindi kwenye mchezo wa kesho.

SOMA NA HII  SKAUTI SIMBA AZIDI KUFICHUA MAZITO..." SIWEZI KULETA MCHEZAJI WA AL AHLY HAPA..." MAYELA ATAJWA..