Home Habari za michezo KAMA UTANI MZAMIRU ABEBWA NA PENATI ZA NGAO YA JAMII

KAMA UTANI MZAMIRU ABEBWA NA PENATI ZA NGAO YA JAMII

Habari za Simba sc

ACHANA na ushindi wa penalti wa Simba dhidi ya Yanga kwenye Ngao ya Jamii juzi Jumapili jijini Tanga, ishu kubwa ni namna ambavyo kiungo mzawa, Mzamiru Yassin alivyovaa ujasiri wa kupiga penalti.

Simba na Yanga kwenye mchezo huo wa fainali zilimaliza dakika 90 bila kufungana kisha zikaenda kwenye hatua ya kupigiana penalti.

Ni kama vile wachezaji wazawa katika timu zote waliwaachia wachezaji wa kigeni jumba bovu la kupiga penalti katika mchezo huo ambao ulikuwa umeteka hisia za mashabiki wengi wa soka nchini.

Mzamiru amegeuka kuwa shujaa kwa wazawa kwani ndiye mchezaji pekee aliyepiga mikwaju hiyo ya penalti na kufunga na hilo sio tu kwa timu yake Simba bali hadi upande wa Yanga.

Kiungo huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua mikwaju ya penalti kwa upande wa Simba na aliweka wavuni huku kipa wa Yanga, Djigui Diara akiruka upande mwingine na mpira kwenda kwingine.

Upande wa Yanga, Stephen Aziz Ki ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga penalti na aliweka wavuni.

Wachezaji wengine waliopiga penalti upande wa Simba ni raia wa Burundi, Saido Ntibazonkiza, alikosa, Moses Phiri (Mzambia, alikosa), Mcameroon Willy Onana na raia wa DR Congo, Jean Baleke ambao walipata. Upande wa Yanga wengine waliopiga mikwaju ya penalti ni raia wa Uganda, Khalid Aucho na Waivory Coast, Pacome Zouazoua na Yao Attohoula ambao wote walikosa.

SOMA NA HII  KOCHA AS VITA SALUTI...KUWAVUSHA YANGA NUSU FAINALI SHIRIKISHO

1 COMMENT