Home Habari za michezo GAMONDI:- SINA PRESHA NA SIMBA ….TUTACHEZA KAMA TUNAVYOCHEZAGA NA IHEFU….

GAMONDI:- SINA PRESHA NA SIMBA ….TUTACHEZA KAMA TUNAVYOCHEZAGA NA IHEFU….

Habari za Yanga SC

Zikisalia siku nne tu kabla ya mchezo wa watani wa jadi, Simba SC na Young Africans, Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Angel Gamondi, amesema hana shaka na wachezaji wake katika kutimiza majukumu yao kwenye mchezo huo na hataki kuwapa presha.

Gamondi, amesema anafahamu mchezo dhidi ya Simba SC ni tofauti na michezo mingine, lakini hataki kuwabebesha mzigo wa presha wachezaji wake na badala yake anaendelea kuwapa mbinu zitakazowasaidia kufanya vizuri.

Amesema ameifuatilia Simba SC katika michezo mingi, hivyo anafahamu nini cha kuwapa wachezaji wake katika kukabiliana nao siku hiyo ya mchezo.

“Presha itoke kwa mashabiki labda, lakini mimi nauchukulia mchezo huu kama michezo mingine (ukiwemo dhidi ya ihefu) ingawa ni kweli ni mechi kubwa sana katika Ligi ya Tanzania, nataka wachezaji wangu wafanye kila wanachokifanya kila wakati kwenye michezo mingine, hii itasaidia kupunguza presha kwa wachezaji na kuwapa nafasi ya kutimiza majukumu yao,” amesema Gamondi.

“Tunataka kushinda Jumapili hilo ndilo jambo la msingi, tulipoteza kwa Penati kwenye mchezo wetu wa Ngao ya Jamii, tunaendelea kujipanga na kuwapa wachezaji mbinu zitakazotusaidia kupata ushindi, amesema Gamondi.

Aidha, Kocha huyo raia wa Argentina, amesema anafurahishwa na namna wachezaji wake wanavyojituma mazoezini na haoni presha yoyote kwao.

“Naomba tu mashabiki wetu waendelea kutusa sapoti, naamini utakuwa mchezo mzuri, tutacheza katika ubora wetu na katika mipango yetu,” amesema Gamondi.

Simba SC itakuwa mwenyeji wa Young Africans kwenye mchezo huo wa Ligi KuuTanzania Bara utakaochezwa Jumapili (Novemba 05) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 11 jioni.

Kwa upande wa Kiungo wa Young Africans, Mudathir Yahya, ametamba kuwa hawako tayari kuona wanapoteza kwa mara nyingine tena kwenye mechi hiyo ya Watani wa Jiadi.

Tangu msimu uliopita Young Africans imepoteza mara mbili, ikiwamo mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ngao ya Jamii uliyopigwa Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga na Simba SC walitwaa ubingwa huo kwa mikwaju ya Penati.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mudathir amesema baada ya mchezo wao na Singida Fountain Gate FC, Kocha Gamondi amefanyia kazi madhaifu yao na ubora wa Simba SC.

SOMA NA HII  BREAKING:YANGA YAMTAMBULISHA KIPA MWINGINE TENA