Home Habari za michezo HAO SIMBA HUKO SUPER LEAGUE, HAPA AL AHLY PALE MAMELODI SIO POA

HAO SIMBA HUKO SUPER LEAGUE, HAPA AL AHLY PALE MAMELODI SIO POA

Habari za Simba

Droo ya African Football League (Super League) inatarajiwa kufanyika Septemba 2 huko Misri.

Simba Sc ni miongoni mwa timu nane ambazo zitashiriki michuano hiyo maalum ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Timu zimewekwa katika makundi mawili ya timu nne kulingana na alama walizokusanya katika mashindano ya CAF miaka mitano iliyopita.

Kundi A lina timu za Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Wydad Athletic na Esperace. Kundi B lina timu za Simba, TP Mazembe, Enyimba na Perto Luanda.

Timu za kundi moja hazitakutana kwenye hatua ya awali kwa maana timu kutoka kundi A itapangwa kuchuana na timu kutoka kundi B.

Simba itafungua michuano hiyo Oktoba 20 kwa kuchuana na Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Wydad au Esperance.

SOMA NA HII  KIMEUMANA CHELSEA....TUCHEL NAYE 'KALIWA KICHWA' MCHANA HUU...