Home Habari za michezo JEMEDARI AWASAGIA KUNGUNI YANGA KISA FEI TOTO

JEMEDARI AWASAGIA KUNGUNI YANGA KISA FEI TOTO

Habari za Azam FC

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said Bin Kazumari ameonyesha kuwashangaa mashabiki wa Klabu ya Yanga kufuatia vitendo vyao vya kumzodoa aliyekuwa mchezaji wao, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’.

Hii inakuja baada Fei Toto kuwanyoshea kidole mashabiki wa Yanga baada ya kufunga penati kwenye mchezo wao wa CAF dhidi ya Bahiri Kanema lakini mwisho wa siku Azam ilipoteza mchezo huo na kufungashiwa virago rasmi kwenye mashindano ya CAFCC.

Baada ya tukio hilo, mashabiki wa yanga walianza kumzodoa Fei mitandaoni wakisema kuwa ana kiburi ndiyo maana timu yake imeshindwa kufika mbali kwenye mashindano ya kimataifa.

“Kitu kimoja ambacho sijaridhika na watu Yanga, kwenye maisha tunasema ukishikwa shikamana, ukiachwa achika. Mashabiki wa Yanga wakubali kwamba Fei Toto sio mchezaji wao, hii habari ya kuanza kumsema kila anachofanya wanakosea.

“Fei ni kijana wetu, ameangalia maisha yake akaona atayapata Azam. Timu yake imeshacheza imetolewa, ameshamaliza, … heti huyu mtoto ana mdomo sana, ana kiburi ana maneno sijui nini…

“Jamani mambo ya kusema yule mwanamke nilikuwa nampeleka vacation Dubai, yeye ameshakubali kwenda Kzimkazi na mumewe mpya, jamani achikeni,” amesema Jemedari Said.

SOMA NA HII  AHMED ALLY AWEKA WAZI ISHU YA KIMATIFA