Home Azam FC KAULI HII YA SOPU KWA AZAM FC NI KAMA MASTAA ULAYA WANAVYOFANYAGA...

KAULI HII YA SOPU KWA AZAM FC NI KAMA MASTAA ULAYA WANAVYOFANYAGA WAKISAJILIWA TIMU MPYA…


Baada ya kusajiliwa Azam, straika, Abdul Sopu ameahidi kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo kwa msimu ujao.

Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha kubwa kutokana na kiwango alichoonyesha akiwa na timu ya Coastal Union ya Tanga.

Sopu alikuwa mchezaji nyota kwenye mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho, huku akifanikiwa kufunga goli tatu kwenye mchezo huo.

Akizungumzia hilo, Sopu amesema kuwa “Ni furaha kubwa kwake kujiunga na klabu hiyo na haukuwa uamuzi mgumu kwa upande wake.

“Kujiunga na Azam haikuwa ngumu kwangu kwani ni timu yangu ya nyumbani, ni furaha kubwa kwangu kuwa hapa nawaomba mashabiki watusapoti kwani tumepanga kuwapa furaha kwa msimu ujao.”

Mara nyingi mastaa wa Ulaya wanaposajiliwa na timu nyinginezo, hata kama itafahamika kuwa walikuwa ni wapenzi wa klabu fulani, utasikia wakisema hizo timu walizosajiliwa ni timu zaopendwa toka walipokuwa wadogo, kauli ambayo mara nyingi huonekana ni ya ‘kimchongo mchongo’ hivi.

SOMA NA HII  ISHU YA YANGA SC NA JOB YAFIKIA MWISHO...DILI LA KUTAKIWA NA WAMISRI UKWELI UKO HIVI...