Home Habari za michezo BAADA YA KUONA ‘VIBE’ LAKE LINASHUKA…MANARA AJA NA ‘KISANGA’ HIKI KIPYA MJINI…

BAADA YA KUONA ‘VIBE’ LAKE LINASHUKA…MANARA AJA NA ‘KISANGA’ HIKI KIPYA MJINI…

Mkutano Mkuu Simba leo

Ofisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Sunday Manara amesema yeye amezaliwa kuwa maarufu kwa hiyo si rahisi kwa mtu yeyote kuififisha nyota yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika; “Wakati wa kuzaliwa kwangu, nchi hii ikiwa na magazeti mawili tu ya Kiswahili na Kingireza Uhuru na Daily News, yaliandika stori ya Sunday Manara apata Mtoto wa kiume, kumbuka hyo miaka kuandikwa gazetini ilikuwa ni ujiko kweli kweli.

“Imagine mimi nimeandikwa nilipozaliwa tu, baadae kidogo tu, Magazeti ya Ulaya yakaja na stori ya familia yangu tukitua huko kuutumikia mpira wa miguu, kama picha ya mbele inavyoonekana.

“Miaka michache baadaye tayari napewa microphone kuhutubia hadhira kubwa kubwa, kiufupi nimekuwa prepared toka uzao wangu na media za ndani na nje ya nchi, haikuja kwa bahati mbaya.

“Mic zikiniona tu zinasema Shkamoo Bugati ????. Ukisikia TBT ndio hzi sasa, halaf anatokea Nyantulindi ambae hadi leo anatumia kamba za katani kufungia viatu anataka kushindana na Bugaaaaaa…. yieeee ????????

“Born To be A Star, umashuhuri unatayarishwa mabibi na mabwana. Nb: basi Kuna watakaonuna hadi na tbt za Bugati,,,Uzuri wake sio sheeda zangu,,umnunie nani na maisha umeyaparamia Kwa pupa ????????”

SOMA NA HII  KISA KAULI YA 'KUFA KIUME'....MCHAMBUZI BONGO AWASHUKIA SIMBA SC...."KILA MWAKA WANAISHIA HAPO HAPO TU"...